TAWCA YALIA NA UPUNGUFU WA WAHASIBU NCHINI YATANGAZA MIKAKATI KUONGEZA WIGO

 

TAWCA wakiwa katika matembezi ya hisani katika mitaa ya jiji yaliyoanzia Shule ya Sekondari Azania Uhasibu House, Salenda, Tambaza Sekondari na kuhitimisha Azania Sekondari


DAR ES SALAAM

Na Pilly Kigome

CHAMA cha Wahasibu Wanawake Tanzania (TAWCA) kimefanya matembezi ya hisani kwa lengo la kukuza taaluma kwa kulenga kununua vitabu vya taaluma hiyo katika shule za sekondari na vyuo nchini.

Ikiwa na pamoja na lengo  kuongeza wigo kukuza taaluma ya uhasibu kwa wanafunzi vijana na wasichana ikiwemo na kuwafikia wanafunzi wasioona kwa kuwaandalia vitabu maalumu vya nukta nundu.

Hayo yamesemwa Novemba 4 mwaka huu, jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Hazina ndogo kutoka Wizara ya Fedha,CPA. Evance Asenga wakati akizungumza na vyombo vya habari wakati wa matembezi ya hisani yaliyoandaliwa na Chama hicho kwa ajili ununuzi wa vitabu vya taaluma kugawa katika shule za Serikali.

CPA.Asenga amesema Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na TAWCA imejipanga kujikita kukuza na kuongeza idadi ya wahasibu wanawake nchini bila kusahau makundi maalum ambayo yameonekana kusahaulika katika upatikanai wa vitabu taaluma.

Pamoja na kukuza uchumi wa Tanzania ikiwemo na kuongeza weledi na vipaji kwa wahasibu wanawake kwani kumekuwa na upungufu mkubwa wa wahasibu nchini hasa katika uhakiki wa hesabu na mapato ya Serikali. 

“Changamoto bado zipo idadi ya wahasibu ni ndogo hasa katika taasisi za Umma hasa mapato na matumizi na tunajitahidi kuongeza taaluma kwa bidiii zote ili kufikia lengo” Asenga

Wanafunzi skauti wa kike katika matembezi hayo

Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu za Serikali, Prof.Sylvia Temu, amesema kuelekea siku ya maadhimisho ya Uhasibu Duniani itakayofanyika Novemba 10 mwaka huu,  bodi hiyo imekuja na matembezi hayo yanayolenga kutafuta michango ya kununua vitabu vya uhasibu na fani zinazoshabihiana na uhasibu kwa ajili kugaiya shule za sekondari ili kukuza taaluma.

Amesema wanaamini kufanya hivyo kutachangia kwa kiasi kikubwa jitihada katika kuboresha elimu ikiwemo na kuhamasisha wanafunzi wa kike kutorudi nyuma katika kubobea katika masomo hayo.

Prof.Temu Sylvia,Mwenyekiti Bodi ya Taifa ya Wahasibu akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya matembezi

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu Tanzania CPA.Dr.Neema Kiure amesema ununuzi wa vitabu hivyo vitakavyogaiwa shule za sekondari na vyuo ni kampeni maalum ya kuondoa dhana potofu kwa wanafunzi wa kike inayowaaminisha kuwa fani hiyo ni ngumu na fani ya wanaume pekee.

Amefafanua taasisi hiyo ilianzishwa mwaka 2015 iliyoanza na wanachama 15 ikiwa na lengo la kuidhinisha wanawake wahasibu na kipindi hicho walikuwa kama asilimia 20 nchi nzima.

Ameendelea kufafanua kuwa, kwa sasa nchini kuna wahasibu waliobobea zaidi ya 12,000 lakini wanawake ni asilimia 30 tu.

“Tayari mwaka jana tulishagawa vitabu vya taaluma katika shule ya Tuliani,Makurumla za jijini Dar esSalaam na Iyela ya mkoani Mbeya” amefafanua Kiure

Amesema mbali na uhamasishaji huo taasisi hiyo inajikita na kuinua elimu kwa wanawake na kuanzisha miradi midogomidogo ukiwepo ule uitwao ‘bado naweza’ uliopo Kigamboni.

Mradi huo unalenga kuwaangalia mabinti waliyokatiza masomo kwa kupata mimba za utotoni wanawafundisha ujasiriliamali na biashara ndogondogo na hadi sasa kuna wahitimu zaidi ya 260 katika miradi huo.

Mradi mwingine ni kuwafundisha elimu ya biashara akinamama wajasiriamali kutofautisha mitaji na matumizi binafsi kwani kumekuwa na changamoto kubwa  kwakundi hilowa kula mtaji na kuua kabisa biashara zao.

CPA.Dr. Neema Kiure Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu Tanzania akizungumza na vyombo vya habari kufafanua matembezi hayo


Chapisha Maoni

0 Maoni