PWANI
Na Mwandishi Wetu
MAKAHAMA ya Wilaya ya Lugoba Bagamoyo Mkoani Pwani imemuhukumu Mrisho Hodari Kenya(47) kwenda jela miaka 60 kwa kubaka na kumzalisha mwanae wa kufikia wa miaka 13.
Hukumu hiyo ilitolewa Novemba 9 mwaka huu, mbele ya Hakimu Mfawidhi Samira Suleimani baada ya Mahakama hiyo kujiridhisha na ushahidi pasi na shaka na kumtia hatiani.
Imedaiwa Mahakamani hapo kuwa Oktoba 2021 mshitakiwa alimbaka mwanae Rebeka Felician(12) aliyekuwa akisoma darasa la sita.
Hakimu alihukumu Kesi hiyo yenye namba 237, 2022 kwa makosa mawili la kwanza kubaka, pili kumpa ujazito mwanafunzi huyo .
Hivyo kutokana na makosa hayo kila kosa amehukumiwa miaka 30 jela hivyo kupatikana jumla ya kifungo cha miaka 60.
Kwa kubaka na kukatisha ndoto za mwanafunzi ili iwe fundisho kwa wengine.
Akizungumza na Mtandao huu nje ya Mahakama kwa shida na masikitiko na vilio Mama mzazi wa mwanafunzi aliyebakwa ambaye mke wa mshitakiwa Wivida Alikadi (37) alisema binti alibakwa Oktoba mwaka 2021 wakati yeye akiwa safari jijini Dar es Salaam kumuuguza baba yake mzazi aliyekuwa akisumbuliwa na magonjwa ya moyo.
Wivida amesema mshitakiwa ni mume wake wa ndoa walioana mwaka 2013 Chalinze katika kijiji cha Pingo kipindi hicho mume huyo alimuoa akiwa tayari na watoto wawili wadogo wote wakike ambapo alifafanua mkubwa alikuwa na miaka mitatu na mdogo alikuwa na miezi nane kwa kipindi hicho.
Ameendelea kufafanua kuwa mume wake huyo waliishi maisha ya furaha na amani bila kuonyesha tatizo lolote na hakumnyanyasa kwa namna moja ama nyingine kwani alimshikamkono kwa kumlelea watoto wake hao na watoto walidhani kuwa huyo ni baba yao mzazi kutokana wakati wanaoana hawakuwa na utambuzi wa kumjua baba halisi.
Amefafanua kuwa, Oktoba mwaka 2021 alilazimika kupata safari ya kwenda kuuguza baba yake Majohe Dar es Salaam na kuacha watoto hao kwani walikuwa wakisoma alilazimika kuwaacha nyumbani.
Hivyo kutokana na hali hiyo mumewe alitumia fursa hiyo kumbaka binti mkubwa na kumuelekeza asiseme kwa mtu yeyote atampa zawadi nono na akisema atamuua.
Ameendelea kufafanua katika mahojiano maalum na mwandishi kuwa, wakati akirudi nyumbani kwake alimkuta mwanae huyo akiwa katika hali ambayo si sawa na baadae aligundua kuwa ni mjamzito lakini wakati anajaribu kumuuliza mtoto huyo hakuonyesha ushirikiano na aliamua wamuache kwanza hadi ajifungue kwakuhisi huenda angeweza kusema.
Miezi miwili baadae mama huyo amesema nae alijigundua ni mjamzito hivyo alikuwa akilea ujauzito wa mwanae nae akiwa analea wa kwake pia.
Amesema kuwa baadae hali ya baba yake ikawa bado ni tata na alilazimika kuondoka tena kwa mara ingine jijni Dar es Salaam kuuguza baba yake cha kushangaza huku nyuma mume huyo aliamua kumbaka na yule binti mwingine mdogo ambae kwa kipindi hicho alikuwa na miaka kumi akiwa darasa la pili.
Amesema wakati anarudi nyumbani kwake hapo binti huyo mdogo alimueleza kwamba wakati hayupo nyumbani baba alinibaka ndipo walipoanza kufanya taratibu za kwenda kushtaki polisi na hatua za kwenda kupimwa na daktari alithibitisha binti huyo aliingiliwa.
Amedai kwa kushirikiana na ndugu zake na wasamaria wengine walikwenda kufungua kesi mahakamani lakini cha mume wake huyo mshitakiwa alishinda na kuachiwa huru jambo ambalo amedai liliwashangaza wengi kijijini hapo.
Amesema ndipo binti yake mkubwa nae akaamua kusema ukweli kumwambia mama yake baada ya mdogowake huyo kufunguka na kusema kuwa na yeye hiyo mimba ni ya baba yake huyo.
Ndipo mama huyo alipoamua kufunga virago vyake na kuondoka kwa mume huyo hapo akiwa na watoto watano ambapo mume huyo alibahatika kuzaa nae watoto watatu.
Hivyo kitendo hicho cha mume huyo kufanya vitendo hivyo waliweza kwenda kufungua shtaka lingine mahakamani na hatma yake aliweza kuhumiwa kifungo hicho baada ya mahakama kujiridhisha
“Mwanangu alijifungua June mwaka 2022 sasa hivi mtoto wake mjukuu wangu ana mwaka mmoja na miezi minne” nimefurahi sana Mahakama ilivyomfunga huyu mwanaume kwa nilikuwa inaniumiza sana kuniharibia watoto wangu wote wawili” alifafanua mke wa mshitakiwa
Binti huyo sasa anajifunza ufundi chereheni kwa msaada wa Kituo cha Maarifa na Taarifa cha ‘KC Majohe’ kinachoongozwa na Mwenyekiti Tabu Ali kilichopo chini ya Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP).
“Nashukuru kwa msaada huu kwa mwanangu kujifunza charahani, maana mtoto alikuwa na ndoto za kusoma anikomboe lakini imekuwa bahatimbaya, nawaomba wasamaria wema watakaosikia taarifa yangu waweze kunisaidia japo mtaji niweze kuendesha maisha yangu kwa sasa naishi maisha magumu hayasemeki maana nilikuwa najishughulisha na kilimo pekee, nikipata mtaji angalau niuze chochote niweze kuwalea hawa watoto” amesema kwa machozi mama huyo

0 Maoni