DAR-ES-SALAAM
Na Pilly Kigome
TAASISI ya Human Dignity Tanzania (HDT) kwa kushirikiana na Utu-Networking imeanda tamasha la vyakula vya asili kwa kukutanisha wadau lenye lengo la uhamasishaji wa kuthamini makundi maalum.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Heriety Baragaye amesema tamasha hilo kubwa lina mlengo wa uhamasishaji kuwashirikisha makundi maalum katika shughuli za maendeleo.
Ikiwemo na kuhamasisha kutoa wito kwa jamii ya Kitanzania na duniani kote kushirikiana kutunza mazingira kwa maendeleo ya taifa.
“Utunzaji wa mazingira ni muhimu katika jamaii yetu, na hakuna maendeleo bila ushiriki wa makundi maalum, na hakuna maendeleo bila kuwa na mazingira salama” amefafanua Balagaye
Amefafanua kuwa lengo la kuandaliwa kwa chakula hicho cha pamoja ni kukutanisha wadau wote wanaoguswa na makundi ikiwa na kuweka usawa kwa watu wote bila kubaguana kwani binadamu wote ni sawa.
Amefafanua tamasha hilo linalenga kuandaa vyakula vya asili vya makabila tofauti na makundi maalumu wakiwemo yatima na wajane, wagonjwa walioathirika na virusi vya ukimwi wakiwemo wagonjwa wa saratani na wale waishio mazingira magumu na hatarishi watakutana pamoja.
Tamasha hilo maalum linatarajiwa kufanyika Desemba 2 mwaka huu huko Kibiti mkoani Pwani.
Balagaye alitoa wito kwa yeyote atakayeguswa anaweza akachangia kwani makundi hayo yana uhitaji wa mambo mbalimbali ikiwemo vifa vya shule, mavazi, kukarabati nyumba vyakula, madawa na mengineyo mengi.

0 Maoni