HOSPITALI TEMEKE,TOYOTA WACHANGISHA DAMU

 

DAR-ES- SALAAM

HOSPITALI ya Rufaa Mkoa Temeke imeendesha zoezi la uchangishaji damu kwa kushirikiana na ofisi za Toyota Tanzania ikiwa na lengo la kuisaidia jamii. 

Uchangishaji huo umeambatana na utoaji wa elimu kuhusu umuhimu wa kuchangia damu kwa anaetoa na anae changiwa.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke (TRRH), Dkt. Joseph Kimaro, ameshukuru uongozi wa Toyota Tanzania na kueleza kuwa Toyota wamekuwa wakijitoa mara kwa mara katika kusaidia jamii kupitia uchangiaji damu na kutoa vifaa tiba. 

Kimaro ameeleza awali Toyota vifaa vitasaidia kuokoa maisha ya watoto wachanga, hasa wale wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti) na kuendelea kusema kuwa kwa kujitoa kwao katika kuchangia damu ni hatua nzuri na ya muhimu kwani inaunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya 6 katika kuboresha huduma za afya na hivyo kusaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto katika hatua za awali za ujauzito na baada ya kujifungua. 

Amesema damu hiyo iliyochangishwa ni kwa manufaa ya wagonjwa wa hospitali mbalimbali watakaokuwa na uhitaji na si kwa ajili ya wagonjwa wa Temeke pekee. 

Mkurugenzi wa Hospitali ya Temeke Joseph Kimaro akizungumza wakati wa zoezi la uchangiaji damu

Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Toyota, Bw. Kadiva William, amehimiza wafanyakazi kujitokeza kwa wingi na kuchangia damu.

Amewaeleza kwamba kutoa damu ni kitendo cha ujasiri, kwani inaokoa maisha ya wengine. Hii ni hatua muhimu katika kufanikisha jitihada za jamii na kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya afya.



Chapisha Maoni

0 Maoni