Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati
Dkt. Doto Biteko amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa sekta ya
madini inaendelea kutoa mchango katika ukuaji wa uchumi wa nchi.
Dkt.
Biteko amebainisha hayo leo Oktoba 25, 2023 akifungua Mkutano wa
Kimataifa wa Madini na Uwekezaji Tanzania (TMIF) wa Mwaka 2023 jijini
Dar es Salaam.
“Mpango wa Serikali ni
kuhakikisha kuwa Sekta hii inachangia asilimia 10 au zaidi katika pato
la Taifa ifikapo 2025,” amesema Dkt. Biteko.
Ameongeza
kuwa mchango wa Sekta ya Madini umekuwa ukiongezeka kutoka asilimia 7.3
mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 9.1 mwaka 2022.
Kwamba ukuaji wa Sekta ya Madini kwa mwaka 2022 umekuwa asilimia 10.9 ukilinganishwa na ukuaji wa asilimia 9.4 mwaka 2021.
“Ni
matumaini yetu Sote ifikapo mwaka 2025, Sekta ya Madini itafikia lengo
la mchango wa asilimia 10 kwenye pato la Taifa,” amesema Dkt. Biteko na
kuongeza,
“Mchango wa Sekta ya Madini katika
fedha za kigeni kwa mauzo yote ya bidhaa nje ya nchi umeendelea
kuimarika kutoka dola za Marekani 1.6 bilioni sawa na asilimia 37 mwaka
2018 hadi dola za Marekani 3.4 bilioni sawa na asimilia 47 mwaka 2022,”.

0 Maoni