Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa
Nishati, Dkt. Doto Biteko leo amewasilisha katika Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania azimio la kujiunga na Mkataba wa Wakala wa
Kimataifa wa Nishati Jadidifu (Statute of the International Renewable
Energy Agency - IRENA).
Dkt. Biteko ametaja
manufaa mbalimbali yatakayopatikana baada ya kujiunga na mkataba huo
ikiwemo; kuimarika kwa mchango wa Nishati Jadidifu katika uzalishaji wa
Nishati ya Umeme nchini na kuliwezesha Taifa kuwa na vyanzo
mchanyanyiko vya umeme unaoendana na mahitaji ya ukuaji wa kiuchumi na
kijamii.
Ametaja manufaa mengine kuwa ni
kuimarika kwa uwekezaji, mitaji na upatikanaji wa ushauri wa kiufundi
katika uendelezaji wa nishati jadidifu na kupungua kwa uharibifu wa
mazingira unaotokana na uzalishaji na matumizi ya nishati isiyo rafiki
wa mazingira na pia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
0 Maoni